Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, wamemchagua Joseph Rwegasira (Diwani wa Kata ya Makongo), kuwa Naibu Meya Mteule wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Picha ya kumbukumbu baada ya uchaguzi.

Rwegasira, anachukua nafasi iliyokuwa kishikiliwa na Heri Misinga ambaye muda wake utamalizika mwishoni mwa mwezi huu wa Julai, 2022.

Akiongea mara baada ya uchaguzi huo, Rwegasira amesema, “Ninawashukuru sana waheshimiwa madiwani kwa kuonyesha imani kubwa kwangu, naomba niwahakikishie kwa kushirikiana na Mstahiki meya tutahakikisha tunafanyakazi kwa pamoja ili kuwaletea maendeleo wananchi wetu ndani ya Manispaa yetu ya kinondoni.”

Rwegasira akiwa na Mstahiki Meya, Mnyonge Songoro, Mbunge wa Jimbo la Kawe, Askofu Dkt. Josephat Gwajima na Katibu Mwenezi wa CCM, Mkoa wa Dares Salaam, Simon Mwakifamba.

Habari kuu kwenye magazeti ya leo Julai 21, 2022  
Sheria uhalifu mtandaoni Hatari kwa Wanahabari