Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC, imekutana nchini Namibia kwa ajili ya Mkutano wa pande tatu maarufu kama Troika ambacho ni chombo kinachosimamia masuala ya ulinzi na usalama ya shirika hilo la kikanda, kwa sasa linaongozwa na rais wa DRC ,Felix Tshisekedi.

Mkutano huo, unalenga masuala ya kiusalama mashariki mwa DRC huku ukikazia ombi lake la kutaka kuungwa mkono kijeshi na jumuiya hiyo, katika mzozo na waasi wa M23, ambapo tayari Angola imeonesha nia ya kuunga mkono pendekezo hilo, Lakini Kinshasa inataka uwazi zaidi kwa majirani yake kuhusu swala hili.

Taarifa kutoka Ikulu ya Kinshasa inasema Serikali inampango wa kubadili mamlaka ya vikosi vya Jumuiya ya Afrika mashariki nchini DRC, kwa kuvipa mamlaka ya kushambulia na hakuna haja ya kuwa na viksoi vya kukaa kati kwa kati. Lakini changamoto kubwa kuhusu hili ni kuishawishi Afrika Kusini.

Aidha, Tshisekedi pia alijadiliana na rais Cyril Ramaphosa. Wataalamu wanaona kuwa kinachoelekea ni kutafuta kufufua upya brigade ya kuingilia kati mashambulizi ya waasi iliofaulu kuwasambaratisha M23 mwaka 2013.

Juhudi za kidiplomasia zinaendelea kutafutwa, ambapo baada ya Windhock Rais Felix Tshisekedi ataelekea nchini Botswana kwa safari ya kikazi ambapo atazuru makao makuu ya SADC yaliopo katika mji mkuu wa nchi hiyo, Gaborone.

Ajali ya boti yauwa Watalii 22, utafutaji miili waendelea
Awesu Atoa Funzo kwa Wachezaji wa Ligi Kuu