Kiungo Mshambuliaji wa timu ya taifa ya England na klabu ya Arsenal Bukayo Saka, amekuwa akiandamwa na mashabiki kwenye mitandao ya kijamii ambao wanaonyesha kila dalili za ubaguzi wa rangi.

Hali hiyo kwa mchezaji huyo kinda mwenye miaka 19 imetokea baada ya kukosa penalti kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Italia ya Euro 2020, uliounguruma jana usiku Uwanja wa Wembley jijini London.

Bukayo alitokea benchi na kupewa jukumu la kupiga penati ya tano ambayo ilikuwa ni ya maamuzi Uwanja wa Wembley mwisho wa siku alikosa na kuiwezesha Italia kuwa Mabingwa wa EUFA Euro 2020 kwa kushinda penati 3 huku England ikishinda penati 2.

Ripoti zimekuwa zikionyesha kuwa Mshambuliaji huyo hana bahati kwenye mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na Instagram ambapo jumbe nyingi zinazoonyesha viashiria vya ubaguzi wa rangi zimekuwa zikitumwa na kwenye akaunti yake pia amekuwa akikutana na meseji mbalimbali.

Bahati mbaya pia wengine wamekuwa wakituma emoji kwenye mitandao ya kijamii katika posti ambazo aliziweka muda mfupi kabla ya fainali huku mmoja wa watumiaji alisema kuwa “Ondoka katika nchi yangu na mwingine aliandika kwamba, “Nenda Nigeria”.

Mbali na Saka pia Marcus Rashford pamoja na Jadon Sancho ambao walikosa penati nao wamekutana na jambo hilo.

Shirikisho la Soka la Uingereza, FA imetoa taarifa kwamba itashughulia suala hilo kwa kuwa sio la kimichezo.

Miradi ya bilioni 37 kuzinduliwa Tabora
Nabi aitangazia njaa Ihefu FC