Mwanasheria wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu jana alihojiwa na jeshi la polisi kufutiatia kauli alizonukuliwa kwenye gazeti la Mawio, zinazodaiwa kuwa za uchochezi.

Lissu aliwasili katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi majira ya saa 4 asubuhi na kuelekezwa katika ofisi za makosa ya jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ambapo alikaa kwa takribani saa moja.

Baada ya mahojiano hayo, Lissu aliwaambia waandishi wa habari kuwa kitendo cha kuhojiwa kutokana na maoni yake yaliyochapishwa kwenye gazeti la Mawio lilolofutwa na Serikali, ni harakati za kutaka kumfunga mdomo.

“Wale waliobebwa kwenye uchaguzi leo wanataka kutufumba midomo tusizungumzie masula ya uchaguzi wa Zanzibar kwani machafuko yanaweza kutokea visiwani humo kwa tahadhari hiyo wanatuita wachochezi,” amesema Lissu.

Mbunge huyo aliyeambatana na wanasheria wa Chadema, Peter Kibatala, Fredrick Kiwelo na Hekima Mwasibu alieleza kuwa yeye alichokieleza kwenye gazeti hilo ni tahadhari ya kutokea machafuko visiwani humo, ili hatua za kuzuia ziweze kuchukuliwa mapema na sio vinginevyo.

Alitahadharisha kuwa endapo Rais Magufuli anawajibu wa kuingilia mgogoro huo na kwamba, atawajibika kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kama machafuko yatatokea.

Lissu alieleza kuwa baada ya mahojiano hayo, Polisi walipeleka jalada lake kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), na kwamba atajulishwa kama jalada litafikishwa mahakamani.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro alipoulizwa kuhusu sakata hilo, alisema kuwa hawezi kulizungumzia kwa wakati huo kwani hakuwepo ofisini kwa siku nzima.

 

Wivu wa mapenzi waliua kundi hili kubwa la Muziki nchini
Jack Cliff, aliyefungwa China kwa dawa za kulevya aandika barua ya wazi, iko hapa