Kiungo wa klabu bingwa nchini Italia Juventus FC Sami Khedira ameorodheshwa kwenye orodha ya wachezaji wanaopigiwa upatu wa kujiunga na klabu nguli za soka nchini Marekani.

Khedira mwenye umri wa miaka 29, jina lake limeorodheshwa katika klabu za LA Galaxy, New York City FC na New York Red Bulls, ambazo zimeonyesha kuwa tayari kuiwania saini yake wakati wa dirisha dogo la usajili.

Mtendaji mkuu bodi ya usimamizi wa ligi ya nchini Marekani (MLS) Dan Courtemanche, amesema endapo usajili wa kiungo huyo utafanikishwa kama inavyotarajia, ligi hiyo itaenedelea kujizolea umaarufu duniani kwa kuwa na wachezaji nyota.

Amesema ni mapema kuamini uwezekano wa kukamilishwa kwa mpango wa usajili wa kiungo huyo kutoka nchini Ujerumani, lakini aliposikia taarifa za klabu hizo kumuwania Khedira alijihisi faraja.

Hata hivyo klabu za LA Galaxy, New York City FC na New York Red Buls zitakua na kazi ya ziada ya kufanikisha azma ya kumng’oa Khedira nchini italia, kufuatia mkataba wake kusaliwa na miaka miwili.

Khedira alijiunga na Juventus mwaka 2015 akitokea kwa mabingwa wa soka barani Ulaya klabu ya Real Madrid.

Antonio Conte Aomba Msaada Wa Mashabiki
Gerard Pique Ahofia Kupoteza Ubingwa