Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi 33 Bilioni kwa ajili ya kuwawezesha vijana kufugaji samaki, watakaonufaika na uchumi wa buluu uliopo kwenye ukanda wa Ziwa Viktoria.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega katika ziara yake aliyoifanya Wilayani Buchosa, Mkoani Mwanza Agosti 2022.

Akiongea na vijana hao, ambao wamepata mafunzo ya ufugaji samaki katika vizimba, amesema fedha hizo ni fursa kwa vijana kujipatia ajira ili kuondokana na utegemezi wa uvuvi wa asili.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (watatu kutoka kulia), akipata maelezo juu ya ufugaji wa Samaki.

Naibu Waziri Ulega amesema, “Vijana tujipange na tuchangamkie hii fursa ya kufuga samaki ili tuondokane na tatizo la ajira, tuzalishe samaki kwa wingi ili chakula kiongezeke na tuuze nje ya nchi.”

Hata hivyo, Waziri Ulega amesema lengo la Serikali kupitia mradi huu ni kuzalisha tani Elfu Arobaini za samaki, ambazo zitaongeza uzalishaji kutokana na mahitaji ya samaki kuwa mengi.

TAWA yatumia 'Marathon' kutangaza Utalii
Wakandarasi wababaishaji kusitishiwa mikataba