Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameiongezea kiasi cha shil. 300 milioni Hospitali ya Taaluma ya Tiba ya Mloganzila kutoka mil. 600 hadi kufikia mil. 600 kwaajili ya kukabiliana na changamoto za upungufu wa dawa hospitalini hapo..
Akizungumza katika Hospitali hiyo ya Chuo Kikuu na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas) amewataka wahusika wahakikishe wanatumia vizuri fedha wanazozipata kwa kutatua changamoto za ukosefu wa dawa.
Aidha, Samia amemuagiza Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuongeza milioni 300 ili hospitali hiyo iweze kujiendesha na kuondoa changamoto hiyo.
“Tatizo hata pesa mliyopewa mwanzoni mkichukua dawa MSD hamrudishi tena fedha kule, hakikisheni hizi fedha tunazowapa mlipe bili MSD ili iweze kuleta dawa nyingi zaidi,”amesema Samia Suluhu Hassan
Hata hivyo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Said Abood amesema kuwa wamekuwa wakipata asilimia 24 tu ya dawa ambazo wamekuwa wakizihitaji kutoka Bohari Kuu ya Dawa MSD.
-
Video: Watu wanapewa Ugali na mchuzi wa Maharage wenye punje tano Magereza- Sugu
-
Video: Mkuchika kula sahani moja na wanaokwamisha mafao
-
Video: Serikali ilinifunga jela kwasababu inaniogopa- Sugu