Sanamu la mchezaji na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Barcelona, Leonel Messi lililojengwa nchini Argentina katika mji wa Buones Aires, limeshambuliwa na kuharibiwa na watu wasiyo julikana.
Sanamu la mchezaji huyo mshindi mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or limekutwa limeharibiwa kwa kuvunjwa huku likisalia kiatu tu katika eneo hilo.
Hii ni mara ya pili kushambuliwa kwa sanamu hilo lililojengwa katika eneo ambalo yapo mengine ya wanamichezo mbalimbali kama wa NBA na bingwa wa Olympic Manu Ginobili na legendari wa Hockey, Luciana, mwanzoni mwa mwaka huu lilifanyiwa marekebisho kufuatia kuaharibiwa.
-
Zanzibar Heroes yafanya kufuru Kenya
-
Video: Man United yaichakaza CSKA Moscow
-
Droo ASFC kufanyika ‘LIVE’ kesho
Messi mwenye umri wa miaka 30,licha ya kuisaidia timu yake ya taifa kufuzu michuano ya kombe la dunia hapo mwakani nchini Urusi na kuwa na jumla ya mabao 61 katika michezo 123 aliyoichezea Argentina, mashabiki wanashindwa kuona mchango wake ukilinganisha na akiwa Barcelona kutokana na kushindwa kuipatia kombe la Dunia.