Timu ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imeanza vizuri michuano ya Kombe la Mataifa Afrika baada ya hapo jana kuonyesha matumaini makubwa ya kuwabana mabingwa watetezi wa kombe hilo timu ya Mali kutoka suluhu ya bila kufungana.
Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua Serengeti Boys walionyesha kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu huku wakijilinda katika kila idara katika mechi hiyo ya Afcon, michuano inayofanyika nchini Gabon.
Aidha, Serengeti Boys, ilifanya mashambulizi ya kushtukiza huku wakitumia muda mwingi kujilinda na mipango ya timu ya Mali ambayo ilikuwa inaonekana kuwa na uzoefu wa mashindano hayo.
Hata hivyo, Sare hiyo imeifanya Serengeti boys kuanza vizuri kwa michuano hiyo kwa kujinyakulia pointi moja katika mchezo wa kwanza hivyo kuwa na matumaini ya kusonga mbele.  

Video: Magufuli ang'oa mzizi wa miaka 44 Dodoma, Waziri wa JK atishwa kwa risasi
Magazeti ya Tanzania leo Mei 16, 2017