Serikali imekanusha madai ya baadhi ya watu kuwa kitendo cha serikali kuipa mahakama kiasi cha shilingi bilioni 12.3 kwa ajili ya kushughulikia kesi 400 za kukwepa kodi kuwa ni sawa na kuihonga mahakama ili iipendelee.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango aliwaambia waandishi wa habari kuwa fedha hizo zilitolewa na serikali sio kwa lengo la kuishawishi mahakama bali kuisaidia katika utekelezaji wa majukumu yake kwa kutatua tatizo la uhaba wa fedha katika kada hiyo.

“Mahakama iko huru sana, na serikali haina usemi kwa maamuzi yaliyotolewa na mahakama, ambayo yatakuwa ya aina yoyote,” alisema Dk. Mpango katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, uliohudhuriwa pia na Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe.

Dk. Mpango alieleza kuwa kiasi hicho cha fedha zilizoahidiwa na Rais John Magufuli, tayari zimeshawekwa kwenye akaunti ya Mahakama iliyoko Benki Kuu ya Tanzania.

Fahamu Vyama vilivyosusia uchaguzi wa Marudio Zanzibar na vitakavyoshiriki
Mramba aishauri serikali kuhusu namna ya kuwatumia wafungwa kama yeye