Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW), limesema Serikali ya nchi ya Ghana inapaswa kuchukua hatua za haraka za kukomesha vitendo vya kuwafunga watu wenye matatizo ya afya ya akili.

HRW, imesema vitendo hivyo vinaendelea licha ya kuwepo kwa Sheria ya Afya ya Akili iliyopasishwa miaka 10 iliyopita na inayobaini kuwa watu wenye matatizo ya afya ya akili hawapaswi kufanyiwa vitendo vya ukatili.

Askari Magereza nchini Ghana wakizungumza na wafungwa. Picha ya Ghananian Times.

Ghana, inadaiwa haikuchukua hatua za kutosha kuhakikisha utekelezaji wa sheria hiyo na Mkurugenzi wa haki za walemavu katika shirika la HRW, Shantha Rau Barriga akisema kuwafunga watu wenye matatizo ya akili katika kambi za maombi na vituo vya uponyaji ni aina mojawapo ya mateso.

Hata hivyo, Naibu Waziri wa Afya wa Ghana, Tina Gifty Mensah amesema Serikali haikufurahishwa na vitendo hivyo na kwamba inafanya jitihada za kila aina kuhakikisha inakomesha vitendo hivyo na kuwachukulia hatua stahiki wahusika.

Gwiji la Ujerumani lang'atuka
Roberto Martínez abwaga manyanga