Serikali, imekabidhi eneo la ujenzi wa majengo ya kituo cha Taifa cha kudhibiti Maafa kwa Mkandarasi, Kiure Engineering Limet, lilipo Nzunguni Jijini Dodoma ukihusisha ujenzi wa majengo ya maghala kwa awamu ya kwanza inayoendelea kwa sasa.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, wakati wa Hafla ya makabidhiano ya kituo hicho, Mkurugenzi wa Utawala na Rasimali watu kutoka Ofisi hiyo, Stella Mwaiswaga amesema mradi huo wa ujenzi wa kituo hicho, ambapo katika awamu ya pili utahusisha majengo ya maghala na majengo mengine ya uendeshaji yatajengwa kulingana na upatikanaji wa fedha.
Amesema, Ujenzi huu wa awamu ya pili unaotarajiwa kukamilika kwa kipindi cha miezi kumi na mbili, utagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi 8,850,000,000 ikiwa ni gharama za mkandarasi zinazojumuisha kodi ya ongezeko la thamani, VAT.
Awali akiongea katika makabidhiano hayo, Mhandisi wa mradi kutoka Ofisi ya waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu, Joseph Muhamba alisema lengo la serikali ni kuwa na kituo hicho ili kuwawezesha watendaji wake kufanya kazi katika mzingira wezeshi.