Vyombo vya Usalama vya Serikali ya Congo-Brazzaville vimekanusha madai ya uwepo wa jaribio la mapinduzi dhidi ya Rais wa Taifa hilo, Denis Nguesso aliyeongoza nchi hiyo kwa miaka 39.

Kanusho hilo, linafuatia ripoti katika mitandao ya kijamii ambazo hazijathibitishwa kuwa jeshi lilikuwa likijaribu kumuondoa madarakani Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 79, ambaye kwa sasa yuko New York kwa kikao cha 78 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Denis Sassou Nguesso, Rais wa Congo-Brazzaville.

Tovuti ya Serikali pia ilichapisha taarifa ya kukanusha ripoti za jaribio la mapinduzi. Kumekuwa na wimbi la mapinduzi barani Afrika katika miezi ya hivi karibuni, huku ya hivi punde zaidi katika nchi jirani ya Gabon.

Denis Sassou Nguesso, aliingia madarakani katika nchi hiyo ya Afrika ya kati inayozalisha mafuta wakati wa mapinduzi ya kijeshi mwaka wa 1979 na alipoteza uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi nchini Kongo mwaka 1992, lakini akapata tena mamlaka mwaka 1997 baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Azam FC yaivutia kasi Singida Fountain Gate
Bunge la Tanzania, Morocco kuunda ushirikiano