Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetenga kiasi Cha shilingi bilioni 41.87 kwa ajili ya kusambaza umeme kwenye vijiji 399 mkoani Rukwa.
Ameyasema hayo Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani wakati wa uzinduzi wa utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini awamu ya tatu mzunguko wa pili katika kijiji cha Lowe kata ya Lusaka Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa.
Waziri Kalemani amesema kuwa, Serikali imetenga jumla ya shilingi Trilioni 1.24. kwa ajili ya kukamilisha utekelezaji wa mradi wa umeme Vijijini awamu ya tatu mzunguko wa pili hadi kufikia mwaka 2022.
Hata hivyo Tanzania imefikia asilimia 86 ya usambazaji wa umeme katika vijiji na kuifanya kuwa ya kwanza Afrika kwa kusambaza umeme vijijini.