Nchini Hispania katika jiji la Madrid, mwaka wa 2010 yalianzishwa mashindano ya kulala ambapo washiriki walitakiwa kuonyesha uwezo wao wa kupata usingizi mzito ndani ya dakika 20, ili kuibuka na ushindi.
Mashindano hayo hufanyika baada ya chakula cha mchana, na mshindi huzawadiwa pesa zipatazo kiasi cha zaidi ya Shilingi 2.7 Milioni na zawadi nyingine.
Waandaaji wanasema lengo la shindano hilo ni kukuza uelewa kwa watu juu ya umuhimu wa usingizi na kuwaonesha wale wanaofanya kazi kwa muda mwingi hadi kusahau kupumzisha mwili namna wanavyotakiwa kufanya.
Wamesema ni wazi kuwa kupitia mashindano hayo yametoa taswira kwamba inawezekana mtu kujilazimisha kupata usingizi kwa faida ya afya ya mwili na akili.