Kiungo wa Kimataifa wa Zambia na Klabu ya Simba SC , Clatous Chama anatarajiwa kurejea nchini kesho Juni 10 mchana ili kuungana na wachezaji wenzake kwa maandalizi ya mechi za mwisho za Ligi Kuu Bara. 

Chama aliondoka nchini wiki kadhaa kwa mapumziko mafupi sambamba na kujiuguza jeraha alililonalo na kumaliza matatizo ya kifamilia aliyokuwa nayo, ikiwamo kwenda kuadhimisha mwaka mmoja wa kumbukumbu ya kifo cha mkewe, Mercy Chama aliyefariki dunia Mei 29, 2021. 

Kiungo huyo aliyerejeshwa nchini kutoka RS Berkane ya Morocco katika dirisha dogo baada ya timu hiyo kumsajili awali mwishoni mwa msimu uliopita, aliondolewa kikosi cha Simba siku chache kabla ya mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) dhidi ya Yanga. 

Chama atarejea kesho (Ijumaa) Mchana nchini na moja kwa moja ataenda kambini kujiunga na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mechi tano zilizobaki kukamilisha msimu huu. 

Kiungo huyo tangu arejee Msimbazi amefunga mabao manne na kuasisti moja katika ASFC, huku kwenye Ligi Kuu amefunga mabao matatu, licha ya kushindwa kutumika mara kwa mara chini ya Kocha Pablo Franco aliyetupiwa virago vyake Simba hivi karibuni. 

Majaliwa aridhishwa ujenzi wa Ikulu Chamwino
Wagonjwa wasiojiweza kutibiwa bure