Klabu ya Simba SC imetangaza kuingia Mkataba na Kapuni ya michezo ya kubashiri ya M-bet kama Mdhamini Mkuu kuanzia msimu ujao wa Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ na Michuano ya Kimataifa inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.

Simba SC imetangaza kuingia Mkataba wa Kampuni ya M-Bet, baada ya kumaliza mkataba na Kampuni ya SportPesa uliodumu kwa miaka mitano iliyopita.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kwenye kurasa za Mitandao za Klabu hiyo Kongwe katika Ukanda wa Afrioka Mashariki na Kati, Simba SC imeingia Mkataba wa miaka mitano na Kampuni ya M-Bet, na ufafanuzi zaidi utatolewa na pande hizo mbili katika Mkutano wa Waandishi wa Habari Agosti Mosi.

Simba SC imethibitisha Mkataba kati yake na Kampuni ya M-Bet ulisainiwa tangu Julai Mosi.

Kampuni hiyo imekua ikiidhamini Klabu ya KMC FC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara tangu msimu wa 2020/21.

George Mpole: Sijui nitacheza wapi msimu ujao
Fiston Mayele: Msimu ujao Sitatetema tena!