Aliyekua meneja wa Man utd, Sir Alex Ferguson amepishana na wachambuzi wengi wa soka duniani kuhusu mafanikio ya klabu ya Leicester City ambayo yamekua yakihusishwa na wachezaji wawili Jamie Vardy pamoja na Riyad Mahrez.

Ferguson, ametoa mtazamo wake kwa kusema wachezaji hao wawili wanachokifanya ni kutimiza jukumu lao kama ilivyo kwa wachezaji wengine katika klabu za soka duniani, lakini kwake anaamini mwenendo mzuri wa  LeicesterCity umekua ukichagizwa na beki kutoka nchini Ujerumani Robert Huth pamoja na Wes Morgan kutoka nchini England.

Babu huyo ambaye kwa sasa amebaki kuwa mtazamaji wa michezo kadhaa katika ligi ya nchini England, amesema kazi kubwa inayofanywa na mabeki hao wawili imekua na mvuto wa aina yake, na imepelekea Leicester City kufikia pahala pa kufikiriwa kuwa mabingwa wa soka msimu huu.

Amesema wawilki hao wamekua wakicheza bila kuchoka tena kwa ushirikiano mkubwa katika kipindi chote cha msimu huu, na wakati mwingine wamekua wakiwahamasisha wengine kupambana hadi mwishoni mwa mchezo husika.

Mzee huyo ambaye aliondoka Man Utd mwaka 2013 baada ya kutwaa mataji 13 ya ligi kuu ya England, pia amezungumzia umuhimu wa Jamie Vardy pamoja na Riyad Mahrez kwa kusema una mantiki kubwa katika klabu hiyo, lakini anaamini kazi wanayoifanya ina tofauti na mshike mshike wanaokutana nao akina Robert Huth na Wes Morgan.

Main ImageBeki Robert Huth kushoto, akiwa na mshirika mwenzake Wes Morgan.

“Kufunga mabao pamoja na kutengeneza mashambulizi ni kazi ambayo kila mmoja wetu amekua akiizungumza katika mchezo wa soka, lakini ukweli wadau wengi wamekua wakishindwa kutambua umuhimu wa wachezaji wanaocheza katika safu ya ulinzi.”

“Ni vigumu kuafikiana na nilichokizungumza lakini, ningependa kumpa zoezi kila mmoja wetu atazame wanachokifanya akina Robert Huth pamoja na Wes Morgan, ni kikubwa mno na ndicho kinachoipa mafanikio Leicester City ya leo.” Alisema babu huyo mwenye umri wa miaka 74

Leicester City, imeendelea kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi ya nchini England tangu mwanzoni mwa mwaka huu 2016, na kwa sasa imetengeneza tofauti ya pengo la point tano dhidi ya Tottenham Hotspur wanaomili point 61 huku nafasi ya tatu ikishikwa na Arsenal wenye point 55.

KNVB Wamuandalia Louis van Gaal Mazingira Mazuri
Emmanuel Eboue Afungiwa Kucheza Soka