Shirikisho la soka duniani FIFA, limemfungia beki wa pembeni kutoka nchini Ivory Coast, Emmanuel Eboue kwa kipindi cha mwaka mmoja, baada ya kubainika anadaiwa na aliyewahi kuwa wakala wake Sebastien Boisseau.

FIFA wamefikia maamuzi hayo baada ya kujiridhisha uwepo wa deni hilo, ambalo Eboue alitakiwa kulilipa ndani ya 120, lakini hakufanya hivyo, hatua ambayo imemsababishia makubwa zaidi katika soka lake.

Hata hivyo beki huyo mwenye umri wa miaka 32, huenda akapunguziwa adhabu ama kuruhusiwa kucheza soka wakati wowote, endapo atakamilisha malipo hayo kwa Boisseau.

Hatua ya kufungiwa kwa Eboue ambaye aliwahi kuitumikia klabu ya Arsenal, imekuja ikiwa ni siku chache baada ya kusajiliwa na Sunderland, hali ambayo imeanza kutazamwa kama hasara kwa Paka Weusi ambao wanahitaji huduma yake kutokana na janga la kutaka kushuka daraja linalowakabili.

Eboue, alitarajiwa kuwa sehemu ya kikosi katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili ambapo Sunderland watakua wenyeji wa West Brom, baada ya kukosa mchezo dhidi ya Newcastle Utd ambao ulichezwa majuma mawili yaliyopita.

Sir Alex Ferguson Atoa Ya Moyoni Kuhusu Leicester City
Ruud Gullit: Nipo Tayari Kubebeshwa Gunia La Misumari