Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza kufuatiliwa kwa Watumishi sita wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi, ili warejeshe fedha za umma za makusanyo Shilingi 37.3 Milioni na kisha wachukuliwe hatua za kinidhamu.
Majaliwa, ametoa agizo hilo Septemba 23, 2023 wakati akizungumza na mamia ya Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Mashujaa uliopo tarafa ya Bunazi, Wilayani Missenyi, Kagera.
Amesema, “Uongozi wa Mkoa uendelee kuwafuatilia na kuisimamia Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi ili warudishe fedha za makusanyo za mwezi Julai na Agosti, 2023.”
Watumishi hao sita ni Chrispin Mbuga, Andrephnus Kalisa, Nashrath Buyungilo, Lusiana Irunde, Issack Sadick na Willington Mutabilwa ambao ni watoza ushuru wa Halmashauri.