Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, leo Novemba 30, 2020,  amewaapisha wabunge wawili Humphrey Polepole na Riziki Lulida, kwenye viwanja vya bunge Dodoma.

Akiongea baada ya kuapishwa, Polepole amemshukuru Rais Magufuli na kuahidi kuwa sehemu ya Bunge itakayoleta maendeleo kwa umma.

Kwa upande wake Lulida amemshukuru  Rais Magufuli  kwa imani yake kwake na kuahidi kufanya kazi kwa bidii.

“Nitafanya kazi kwa moyo wangu wote, sitamuangusha, nipo hapa kama mbunge niliyeapishwa; sina mengi, nawashukuru wananchi wa Lindi na Watanzania kwa maombi yao,” amesema Lulida.

Wabunge hao wameapishwa hii leo, baada ya jana Novemba 29, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kuwateua kuwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano.

Serikali yatolea ufafanuzi mkanganyiko ajira mpya za walimu
Ndugai: Tutaendelea kuwatambua wabunge 19 wa CHADEMA

Comments

comments