Kinda wa Nigeria, Josh Onomah amesaini mkataba mnono na wa muda mrefu na klabu ya Tottenham inayoshiriki Ligi kuu nchini England.

Mkataba huo utamuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2020 akiitumikia klabu hiyo.

Kinda huyo mwenye miaka 18 ameitumikia klabu hiyo kwenye michezo 14 ya nichuano yote.

Ikithibitisha juu ya taarifa hiyo klabu ya Tottenham Hotspur kupitia kwenye mtandao wake walisema wanatangaza kumsajili mchezaji huyo.

“Tunatangaza kumsajili Josh Onomah amesaini mkataba mpya na klabu mpaka 2020”

Point Tatu Za Ligi Kuu Kuendelea Kutafutwa Wikiendi Hii
Waamuzi Waanza Kunyooshewa Vidole Ligi Kuu