Kiungo kutoka nchini Ufaransa Moussa Sissoko ametajwa kuwa mmoja wachezaji watano wa Tottenham Hotspurs watakaokosa mchezo wa mzunguuko wa pili wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya CSKA Moscow.

Sissoko alilazimika kutolewa nje ya uwanja wakati wa mchezo wa ligi kuu ya nchini Uingereza mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Middlesbrough kufuatia majeraha yaliyokua yakimkabili.

Meneja wa Spurs Mauricio Pochettino amethibitisha kumuacha kiungo huyo aliyemsajili akitokea Newcastle Utd mwishoni mwa mwezi uliopita, katika safari ya kuelekea nchini Urusi.

Wengine ambao wameshinsdwa kusafiri na kikosi cha Spurs kulekea mjini Moscow ni Harry Kane (Kifundo cha mguu), Eric Dier, Mousa Dembele na Danny Rose (Wote wana matatizo ya misuli ya paja).

Spurs wamesafiri kuelekea mjini Moscow huku wakikabiliwa na changamoto ya kuburuza mkia wa kundi E, baada ya kupoteza mchezo wa mzunguuko wa kwanza dhidi ya AS Monaco.

Podolski Amchana Mourinho, Amwambia Hana Utu
Serge Aurier Kutumikia Kifungo Jela