Waziri Mkuu mstaafu ambaye jana alichukua kadi ya uanachama wa Chadema, Frederick Sumaye ameukosoa uamuzi wa rais John Magufuli kuwasamehe watu waliorejesha kiasi cha fedha walichokwepa kulipa kodi.

Sumaye alitoa mtazamo wake huo jana jijini Arusha baada ya kukabidhiwa kadi ya uachama wa Chadema ikiwa ni miezi takribani mitatu tangu alipojiunga na harakazi za Ukawa na kutangaza kuihama CCM.

“Unawezaje kutoa msamaha kwa wezi na wakepa kodi nchini  kwa kuwapa siku saba eti wawe wamelipa madeni yao? Hili ni jambo la ajabu kabisa. Unawezaje kupitisha msamaha kwa wezi na wakwepa kodi? Sumaye alihoji.

“Haya tuliyaona wakati wa sakata la EPA na sasa tunayaona kwenye makontena, wezi wanasamehewa,” aliongeza.

Zaidi ya shilingi bilioni 10 zimekusanywa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kutoka kwa wafanyabishara mbalimbali waliokwepa kodi kupitia makontena yaliyotoroshwa bandarini baada ya rais kutoa siku saba za ‘rehema’.

Baada ya siku hizo kupita (ijumaa), hivi sasa serikali inawasaka wafanyabiashara 15 ambao hawakujisalimisha katika kipindi kilichotolewa na rais Magufuli. TRA imeahidi kuchukua hatua kali za kisheria dhidi yao kama rais alivyoagiza.

Lipumba aweka wazi jinsi Rais Magufuli alivyosaidia Kesi yake Kufutwa
Lowassa Ajibu Makombora ya Kinana, Awataka Wananchi Wamuaibishe