Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa kifo mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 42 ambaye amekutwa amefariki katika nyumba ya kulala wageni katika Manispaa ya Tabora.

Kamanda Jongo amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana katika nyumba ya kulala wageni ya Uyowa.

Nyumba hiyo ipo jirani kabisa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, Kitete.

Amesema chanzo cha kifo chake bado hakijajulikana na kwamba huenda siku zake zilikuwa zimefika.

“Mtu anakufa mahali popote siku zake zikifika na huyu huenda siku zake zilikuwa zimefika, hata hivyo uchunguzi wa chanzo cha kifo chake kutoka kwa madaktari, utaeleza chanzo,”amesema Kamanda Jongo

Africa-Shenzhen Economic & Trade Cooperation and Exchange Series Conference – Dar es Salaam,
Wawekezaji Sekta ya Chumvi watakiwa kuwa chachu kwa wakulima wadogo