Waziri wa Madini, Doto Biteko amekutana na wadau wa chumvi na kukubaliana kuziondoa changamoto zinazowkabili, hii baada ya Wizara kupokea malalamiko kutoka kwa wakulima wa chumvi wa mikoa ya Mtwara na Lindi mwanzoni mwa Agosti 2021

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Abdulkarim Mruma uliopo katika Ofisi za Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzanaia (GST), Waziri Biteko amewataka wawekezaji wakubwa wa Kampuni ya Neelkanth Salt Limited kutoa elimu kwa wakulima wadogo ili waweze kuzalisha chumvi bora itakayokubalika kutumika katika kiwanda chao na hivyo kuwaondolea changamoto ya soko.

Akizungumzia vyanzo vya malalamiko ya wakulima wa chumvi, Waziri Biteko amesema anapata malalamiko kutoka kwa wakulima wenyewe lakini pia anapata malalamiko kutoka kwa wawakilishi wa wananchi ambao ni wabunge na kumsihi mwekezaji Neelkanth Salt Limited kutatua changamoto hizo.

Waziri Biteko amemshauri mwekezaji Neelkanth Salt kupeleka vifaa na wataalamu wa maabara sehemu ya mashamba ili chumvi ipimwe na kutambulika endapo inakidhi vigezo kabla ya kuisafirisha hivyo kuwapunguzia manung’uniko wakulima wadogo.

Awali akiwasilisha malalamiko ya wakulima wa chumvi kwa wajumbe wa kikao, Makamu Mwenyekiti wa  Chama cha  wa wakulima wa chumvi nchini (TASPA) Hamisi Chilinga, amesema kuna mashamba 400 ya chumvi kwa mikoa ya Mtwara na Lindi ambapo wakulima wamevuna lakini wamekosa soko kutokana na mnunuzi Kneelkanth Salt Limited kutoikubali chumvi inayozalishwa na wakulima hao badala yake huagiza chumvi kutoka nje ya nchi.

Tabora: Akutwa amefia gesti
Ambundo asisitiza kurejesha heshima Young Africans