Mshambuliaji wa AS Roma, Tammy Abraham, ameelezea siri ya kuwa imara uwanjani aliyofundishwa na kocha wake wa sasa, Jose Mourinho.

Nyota huyo ambaye alianzia maisha yake ya soka kwenye akademi ya Chelsea hadi alipopandishwa timu ya wakubwa na baada ya kutokupata nafasi ya kucheza mara kwa mara akapelekwa kwa mkopo kwenda klabu za Bristol City, Swansea City, Aston Villa na kurudi tena Stamford Bridge kabla ya kuuzwa kwenda Roma.

Alipoulizwa ni kwa kiasi gani Mourinho amemsaidia, alijibu ni, “kuwa mnyama kweli”, nafikiria kitu kimoja alichoniambia, nilikuwa laini laini na nahitaji kuwa mtu wa nguvu kama mshambuliaji.”

“Si suala la kuwa laini kwenye uwanja, unahitaji kuwa mtu wa nguvu, ili uwapo wako uwaogopeshe mabeki, nadhani hicho ndicho nilichojifunza na naendelea kukifanyia kazi,” aliongezea Abraham.

Abraham kwa sasa ameitwa tena kwenye kikosi cha England katika michuano ya kufuzu Kombe la Dunia nchini Qatar 2022.

Alisajiliwa Roma akitokea Chelsea kwa ada ya pauni milioni 34 na kusaini mkataba wa miaka mitano, huku pia kukiwa na kipengele cha Chelsea kuweza kumnunua tena kwa kiasi cha pauni milioni 68, lakini lazima awe amecheza misimu miwili.

Young Africans yaingia kambini
Donnarumma: Sijazoea hali hii