Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatib
Malimi ameipongeza Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma
(PPRA) kwa kusimamia vizuri Mfumo wa Ununuzi kwa Njia ya
Mtandao (TANePS) na kuhakikisha wanaendelea na Matumizi ya ‘Force
Account’, hatua iliyosaidia kuongeza ukidhi wa sheria na kuokoa fedha
za umma.

Dkt. Kazungu ameyasema hayo alipokuwa akifungua Awamu ya Pili ya
Kongamano la Nane la Usimamizi Katika Ununuzi wa Umma
uliofanyika Mei 1, 2021 jijini Arusha, alipohudhuria kwa niaba ya
Waziri wa Fedha na Mipango.

Aidha, Naibu Katibu Mkuu huyo aliwataka PPRA kuongeza jitihada
katika kutoa elimu kwa watendaji na umma kwa ujumla na kukamilisha
usajili wa taasisi za umma kwenye TANePS kwa asilimia 100, kwakuwa
hadi sasa wameshaunganisha asilimia 98 ya taasisi zote za umma.

“Niwapongeze sana PPRA kwa kazi nzuri mliyoifanya ya kutoa elimu
kwa watendaji na kutoa fursa ya kuendesha mijadala huru na yenye tija.
Natarajia kwamba tutakapokutana mwakani kwenye Kongamano la Tisa
kama hili, nitaona asilimia Mia Moja ya taasisi za umma zitakuwa
zinatumia TANePS katika kuchakata Ununuzi yao,” alisema Dkt.
Kazungu.

Kuhusu matumizi sahihi ya force accouts, Dk Kazungu alisema kuna
faida nyingi za mfumo huo akitoa rai kwawashiriki na PPRA
kuhakikisha changamoto ambazo zinachangia kusuasua kwa matumizi
ya force accounts zinatatuliwa.

“Ni matumaini yangu kuwa baada ya majadiliano katika kongamano hili
changamoto zitakua zimetatuliwa na matumizi ya force accounts
yatakua endelevu” alishauri dk Kazungu.

Awali, Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo,
alisema kuwa hadi sasa Mamlaka hiyo imeshaziunganisha kwenye
TANePS jumla ya taasisi 557 ambazo ni sawa na asilimia 98. Pia,
alieleza kuwa zabuni zenye thamani ya Sh. 24.07 trilioni zilichakatwa
kupitia mfumo wa TANePS hadi kufikia robo ya tatu ya Mwaka wa
Fedha 2020/2021.

“Jumla ya taasisi nunuzi 557, sawa na asilimia takriban 98 ya taasisi zote
nunuzi, zimekwisha unganishwa kwenye mfumo wa TANePS, na jumla
ya wazabuni 19,557 wamekwishajisajili katika mfumo huo, ambapo
mpaka kufikia robo ya tatu ya mwaka huu wa fedha, jumla ya zabuni
39,716 zenye thamani ya TZS Trilioni 24.07 zikiwa zimeorodheshwa au
kuchakatwa kupitia mfumo wa TANePS,” aliongeza.

Aidha, Mhandisi Kapongo alisema kuwa kutokana na hatua hizo
zilizochukuliwa na PPRA chini ya Wizara ya Fedha na Mipango, ukidhi
wa sheria umekuwa ukipanda kila mwaka, ambapo sasa umefikia
asilimia 78.8 kwa ukaguzi uliofanyika Mwaka wa Fedha 2019/2020,
kutoka asilimia 39 wakati ukaguzi wa kwanza wa kutathmini ukidhi wa
sheria ulipofanyika mwaka 2006/2007.

Kwa mujibu wa Afisa Mtendaji Mkuu huyo, PPRA imefanikiwa kuokoa
kiasi cha Sh. 30 bilioni katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2017/18,
ambazo zingepotea kutokana na kutofuatwa kwa taratibu za ununuzi wa
umma.

Wakati huohuo, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya PPRA, Profesa
Sufian Bukurura aliyemuwakilisha Mwenyekiti wa Bodi hiyo, alisema
sekta ya ununuzi wa umma nchini inakabiliwa na changamoto

mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kiwango cha chini cha weledi na
kukosekana kwa uadilifu miongoni mwa Watumishi wa umma na
Wazabuni; na uhaba wa Watumishi wenye taaluma ya ununuzi katika
taasisi zinazoshughulikia masuala ya ununuzi wa umma kuanzia ngazi
ya usimamizi hadi utekelezaji.

Hivyo, aliwataka washiriki wa Kongamano hilo kushiriki kikamilifu
katika mijadala yenye tija, ili kuzitafutia ufumbuzi changamoto
mbalimbali kwenye sekta hiyo, kwa kuzingatia kuwa katika kipindi cha
miaka mitano Sheria ya Ununuzi wa Umma imefanyiwa mabadiliko
mbalimbali.

Kongamano hilo lenye kauli mbiu, “Maboresho ya Mfumo wa Ununuzi
wa Umma Nchini: Mafanikio na Changamoto,” lilihudhuriwa na
washiriki takribani 400 wakiwemo wanasheria wa taasisi za umma,
wenyeviti na wajumbe wa bodi za zabuni na watendaji katika vitengo
vya usimamizi wa ununuzi wa umma (PMU).

Manji mikononi mwa TAKUKURU, sababu za kushikiliwa hizi hapa
Wizara ya Nishati yaombwa kumaliza ujenzi kituo cha kupozea umeme