Mbunge Jimbo la Biharamulo Magharibi, Ezra John Chiwelesa ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Nishati kumaliza utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa kituo cha kupozea umeme kwa kufunga transfoma eneo la Nyakanazi ambazo mpaka sasa transfoma 2 zipo bandari miezi 6 tangu Disemba 20, 2020 kwasababu ya TANROAD na TANESCO wanashindwa kuelewana jinsi gani watalipana ili waweze kuruhusu tansfoma zipelekwe nyakanazi

Chiwelesa ameyaeleza hayo Juni 2,2021 alipokuwa akichangia kwenye uwasilishwaji bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2021/2022 ya Wizara ya Nishati.

Aidha, Chiwelesa ameitaka serikali kutoa mwongozo juu ya mkandarasi Powergen anayetoa huduma ya umeme katika kata ya Nyantakara na Kaniha Wilayani humo ambaye alipewa maelekezo ya kuuza unit 1 ya umeme kwa tsh.100 ila yeye anauza unit 1 kwa Sh 2000.

Shamba la Valeska lafutwa

Wakati huo huo, Chiwelesa ameiomba serikali kama inawezekana aliyepewa kazi ya kutekeleza mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta apewe eneo ajenge kiwanda cha kuzalisha mabomba hayo ili kuondokana na adha ya kutengenezea mabomba hayo sehemu nyingine na kuyasafirisha.

Chiwelesa amesema gharama zinazotumika kusafirisha mambo hayo zaidi ya kilomita 1,000 zinatosha kujenga kiwanda Mkoa wa Kagera, ambacho kitasaidia vijana kupata ajira kwenye hicho kiwanda kuliko kuleta meli nzima ambayo imejaa mabomba na kuongeza gharama za usafirishaji mpaka eneo la utekelezaji wa mradi .

TANePS yasaidia kuongeza ukidhi wa sheria, kuokoa fedha za umma
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Juni 3, 2021