Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA), imetangaza wananchi wa Tanzania kushuhudia tukio la kupatwa kwa mwezi usiku wa leo januari 10, 2020 kuanzia saa 2:17 usiku hadi saa 6:17.

Taarifa hiyo imedai kuwa, tukio hilo litashuhudiwa na nusu ya Dunia ikiwemo sehemu za bara la Ulaya, Asia na Australia.

Imeelezwa kuwa hakuna athari za kibinadamu au hali ya hewa zinazotalajiwa kutokana na tukio hilo na wananchi hawatahitaji kutumia darubini au kifaa chochote ili kushuhudia.

Aidha TMA imetahadharisha kuhusu uwezekano wa kuongezeka kwa kina cha maji katika Bahari wakati wa maji kujaa kutokana na mvutano huo.

Kupatwa kwa Mwezi hutokea wakati Dunia na mwezi vinapokuwa kwenye mstari mmoja.

Mapinduzi Zanzibar: Mama Samia achochea moto afya ya mama na mtoto
Wazazi wamuua mwalimu kwa moto kisa matokeo