Rais Mokgweetsi Masisi wa Botswana amewataka Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania na Botswana kukutana, ili wabainishe mambo yanayotakiwa kufanyiwa kazi ikiwemo corona, masuala ya ulinzi na usalama, elimu na siasa.

Rais Dkt. Masisi ambaye ameanza ziara ya siku mbili hapa nchini ameyasema hayo jijini Dar es salaam, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kikao cha faragha na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan.

Aidha Rais Masisi amesema kuwa ana Imani kubwa na uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuimarisha ushirikiano wa Tanzania na Botswana.

“Nina Imani na Rais Samia Suluhu Hassan, namtakia heri kwa kuwa ni Mwanamke wa kwanza Rais katika nchi za Jumuiya ya SADC, na nipo tayari kutoa ushirikiano wa karibu kwa kuwa historia ya nchi zetu ni kubwa.” amesisitiza Rais Masisi.

Kwa upande wake Rais Samia Suluhu Hassan amesema atatuma watalamu wa Tanzania kwenda nchini Botswana kujifunza namna nchi hiyo inavyofanya vizuri kwenye masuala ya kiuchumi, ili kuja kufanya hivyo hapa nchini.

“Moja ya nchi zenye uchumi imara Afrika ni Botswana, hivyo tuna kila sababu ya kwenda kujifunza huko ili nasi tuweze kufanya vizuri kwenye uchumi wetu.” amesema Rais Samia Suluhu Hassan.

Mbali na uhusiano ya siku nyingi kati ya Tanzania na Botswana, nchi hizo mbili ambazo ni Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zimekuwa na uhusiano wa kiuchumi na Kidiplomasia wa muda mrefu.

Serikali kukopa Sh 7.34 trilioni
Bodaboda, bajaji faini sh 10,000