Ripoti ya Shirika la Kimataifa la Transparency International (TI), Jumanne lilitoa ripoti inayoonyesha hali ya ufisadi duniani kwa mwaka 2018, ambapo mataifa ya Tanzania na Rwanda yameorodheshwa kufanya vizuri katika vita dhidi ya rushwa.
Rwanda ilitajwa kufanya vizuri zaidi kwa kuwa na pointi 56 ikiwa katika nafasi ya 48 wakati Tanzania ikiwa katika nafasi ya 99 kwa kupata pointi 36.
Aidha, ripoti hiyo pia imebaini kuwa Kenya ilishuka kwa pointi moja kutoka mwaka 2017, ambapo ilikuwa na pointi 28, huku mwaka jana ikiwa na pointi 27 na kushika nafasi ya 144 kati ya nchi 180.
Uganda ilipata pointi 26 na kuchukua nafasi ya 149. Burundi iko katika nafasi ya 170 huku Sudan ikiwa katika nafasi ya 172 ikiwa na pointi 16.
Kwa upande wake wenyekiti wa taasisi hiyo, Ferreira Rubia amesema kuwa uimara wa demokrasia katika baadhi ya nchi ndicho kigezo kikubwa cha kufanya vizuri katika nchi ambazo zinapambana na ufisadi duniani.
Hata hivyo, nchi za Denmark na New Zealand zimeongoza katika orodha ya nchi zisizokuwa na kiwango kikubwa cha ufisadi, lakini nchi fisadi zaidi zilizo orodheshwa ni pamoja na Somalia, Sudan Kusini na Syria.
-
Mahakama yamfungia mipaka na benki mpinzani wa Maduro
-
Usalama: Marekani yazihofia Korea Kaskazini, China na Urusi
-
Mahakama yamfungia mipaka na benki mpinzani wa Maduro
Shirika hilo limeeleza kuwa sababu ya nchi hizo kuwa katika kiwango kikubwa cha ufisadi ni vita vya aina moja au nyingine, ikiwa ni pamoja na misukosuko ya ndani ya nchi ambayo imekuwa ikiathiri sana vita dhidi ya ufisadi, amesema mchambuzi wa masuala ya uchumi, Chrispus Yankeem katika mahojiano ya simu na Sauti ya Amerika siku ya Jumanne.