Serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Rwanda zimekubaliana kuimarisha biashara, kuleta mageuzi katika sekta ya usafirishaji na uwekezaji kwa ustawi bora wa pande hizo mbili ambazo ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya Habari jijini Dar es Salaam, imeeleza kuwa mara baada ya kukutana na Rais wa Rwanda, Paul Kagame, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema biashara kati ya nchi hizo mbili haziakisi rasilimali nyingi zilizopo na hivyo kuona
ipo haja ya kutumia miundombinu kukabiliana na changamoto hiyo.

“Lazima kuwe na mageuzi katika sekta hiyo ili nchi hizo mbili ziwe katika nafasi ya kunufaika na rasilimali zilizopo, sasa tunaendelea kuimarisha bandari zetu, hasa Dar es Salaam na Tanga zinazotumiwa pi na Rwanda, tumejadili jinsi ya kuimarisha njia nyingine za mawasiliano ili Tanzania iweze kutoa huduma bora kwa Rwanda na nchi nyingine zinazotuzunguka,” ilieleza sehemu ya taarifa ya hiyo ikimnukuu  Rais Samia.

Kuhusu  Mradi wa Umeme Rusumo uliopo
mpaka wa pamoja kati ya Rwanda na Tanzania eneo la Mto Kagera unaoendelea, Rais Samia amesema, unaendelea vizuri na wamekubaliana kuuzindua kwa pamoja na kwamba vyombo vya usalama vitaendelea kufanya kazi kwa pamoja ili kuimarisha usalama katika nchi hizo na ukanda wa Afrika Mashariki.

Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Paul Kagame amesema, Tanzania ni mshirika mkuu wa Rwanda hasa kwenye
sekta ya usafirishaji na uunganishaji wa biashara na kwamba uwepo wa amani na utulivu ni tunu kwa bara Zima la Afrika na nguzo inayowezesha ustawi wa kijamii na kiuchumi.

Simba SC mguu sawa Morocco, Robrtinho, Mzamiru wafunguka
Mwamnyeto afichua mpango kazi Young Africans