Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA), kimestushwa na kitendo cha mchezaji wa Simba kudaiwa kumpiga mwandishi  kwa masikitiko makubwa kitendo cha wa  habari za michezo la gazeti la Mwananchi, Mwanahiba Richard.

Tumeongea na Mwandishi mwenyewe kujua ukweli, tumemtafuta kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Mika Nyange naye kutaka kufahamu hali ya upelelezi ilipofikia lakini kufanyika haraka kwa uchunguzi ili  haki ya kila mtu ipatikane.

Lakini tumeweza kuzungumza na upande wa pili, kwa viongozi wa Simba kujua kama nao wao wamebaini kosa la mchezaji huyo.Mwenyekiti wa Simba,Evans Aveva ameahidi kutoa ushirikiano na kuomba tusubiri uchunguzi wa

Polisi ndipo upatikane ukweli wa jambo ili.

Sisi kama TASWA tunalaani tukio ili na tumekuwa tukikemea sana vitendo hivi kwa kupiga waandishi, lakini kumekuwa hakuna jitihada zozotew ambazo polisi inalichukua kwa wahusika na badala yake madai kama haya yanapotea.

Kwa kuwa jeshi la polisi limeahidi kutoa ufafanuzi wa upelelezi wa tukio ili haraka iwezekanavyo, naomba waandishi wenzangu pamoja na muathirika wa tukio ili, tuvute subira ili haki ichukue mkondo wake ili sheria ifanye kazi yake.

Taswa itaendelea kulinda heshma ya mwandishi wa habari za michezo na isingepeda kuona mwandishi anaonewa na kudhalilishwa wakati akifanya majukumu yake.

Kwa upande wetu napenda kutoa shukrani kwa nahodha wa Simba, Mussa Hassan Mgosi na kocha wa timu hiyo Jackson Mayanja kwa ushirikiano walioonesha katika tukio hilo na wamedhihilisha uwezo wa kuwaongoza wenzao.

TASWA itakuwa inafuatilia suala ili kwa karibu zaidi.Tupo katika kuhakikisha waandishi anafuata taratibu, sheria za taaluma ya habari.Jambo ambalo Mwanahiba amelifanya kwa kumlinda source wake hadi kupata kipigo .

Juma Pinto
Mwenyekiti TASWA

Adhabu Ya Yondani Yapata Baraka Za Kamati Ya Saa 72
Utafiti: Umaarufu wa Lowassa waporomoka kiasi hiki