Mkutano wa 65 wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani-Kamisheni ya Afrika (UNWTO-CAF), uliofunguliwa rasmi na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jijini Arusha unaendelea kuhusu utalii barani Afrika.
Mkutano huo, wenye kauli mbiu isemayo ” Rebuilding Africa’s Tourism Resilience for Inclusive Socio-Economic Development,” umekutanisha washiriki 200 kutoka mataifa mbalimbali, kujadili masuala yanayogusa shughuli za utalii barani Afrika.

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), imeshiriki kikamilifu kwenye ufunguzi huo wa mkutano ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Meja Jenerali ( Mstaafu), Hamis Semfuko na Kaimu Kamishna wa Uhifadhi, Mabula Misungwi Nyanda.