Shirika la Kutetea Haki za Wanawake Wajane Tanzania (TAWIA), limemuomba Rais Dkt. John Magufuli kuunda wizara ya wajane ili kushughulikia kwa kina matatizo yanayowakabili wajane nchini.
Akitoa rai hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TAWIA, Rose Sarwatt ameelezea umuhimu wa kuanzishwa kwa wizara hiyo.
“Wakati umefika sasa awepo Waziri wa wajane, pia kuwepo na sheria inayomtambua mjane katika masuala ya kijamii, yakiwamo matibabu bure, ” Tanzania Daima limemnukuu Sarwatt.
“Tunaomba sana kundi hili litambuliwe na kuthaminiwa tunaamini serikali itaanzisha wizara hii haraka,” aliongeza.
Sarwatt ameeleza kuwa kama Rais alishaunda wizara inayohusisha wazee, watoto na wenye ulemavu, Wizara ya wajane haitaweza kushindikana kuundwa endapo ataziona faida zake.
Moja ya changamoto wanayokutana nayo wajane iliyotajwa na TAWIA ni kukosekana kwa elimu ya sheria kwa baadhi ya wajane ambayo inasaidia kulinda haki zao, japokuwa ili mjane apunguziwe mzigo wa kupigania haki ni lazima jamii nzima iweze kupata elimu ya sheria kuhusu haki ya ndoa na unyanyasaji wa kijinsia.
-
Lissu auweka ubunge wake rehani, kuzuru Ulaya na Marekani
-
Rais amsimamisha Jaji Mkuu kupisha uchunguzi
Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa wanawake wana wajibu wa kupigania haki na maendeleo yao, ili kukomesha umasikini kwenye kaya zao kwani iwapo watawajibuka kikamilifu na kukataa kuonewa watatokomeza umasikini.