Wasanii wengi kwa sasa wameonekana kuwa na ushindani mkubwa wa mashabiki hasa katika mitandao ya kijamii, Mashabiki hao wamekuwa na msaada mkubwa katika kukuza kazi zao lakini pia ni chanzo cha uadui kwa baadhi ya wasanii.

Wasanii wanaoongoza kuwa na hizo team ni wema sepetu, Shilole, Diamond platnumz, Ali kiba na wengineo wengi, team hizi zimekuwa zikijenga zingne zikikuza chuki kwa wasanii pasipo kuwa na sababu za msingi.

Akizungumza na Mtangazaji wa Kings FM, Divine Msanii Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amewataka mashabiki wote wakiwemo wa kwake wasapoti kazi za wasanii na siyo watumie majina ya watu vibaya kwa kutukana watu mitandaoni.

”mimi siwajui, sina timu yoyote. nina akaunti yangu ya badgirl shishi tu kama watu wanafungua akaunti hizo kwa majina ya watu na  kwa mapenzi yao binafsi basi wasiharibu majina ya watu”. Alisema shilole

Hata hivyo msanii huyo anayetamba na kibao cha’ Say my name’ alicho shirikiana na Barnaba Boy  anayeaminika kuwa na mgogoro na aliyekuwa mpenzi wake Nuh Mziwanda pamoja na mrembo wa video ya jike shupa ”Zuu” amesema yeye hana hawezi kuzungumzia yanayosemwa kwenye mitandao.

“Sihitaji kuongelea hivyo vitu, niulize kuhusiana na muziki wangu, mambo yangu yanavyoenda, usiniulizie vitu vya watu ambao siwajui mimi,” alijibu muimbaji huyo.

 

 

Video: Waziri wa Israel azuru Uganda
Magufuli amtumbua jipu mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya TIB