Chelsea wanaamini winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 20, atajiunga na Manchester United hivyo wamebadilisha gia angani kwa kumnyatia hivi sasa kiungo mshambuliaji wa Bayer Leverkusen Kai Havertz.

The Blues hao wameshafanya mazungumzo na kumsajili kiungo huyo ambapo hata hivyo winga Said Benrahma yupo katika rada za klabu hiyo.

  • Aston Villa pia inahusishwa kumsajili winga wa Algeria Benrahma, 24, ambaye Chelsea watafikiria kumvuta Stamford Bridge.
  • Beki kisiki wa Brazil na Paris Saint Germain Thiago Silva anatajwa kutua katika klabu moja wapo England baada ya zaidi ya vilabu tano kuhusishwa kumchukua mlinzi huyo, Arsenal, Everton, Newcastle, West Ham na Wolves zinahitaji saini ya kitasa huyo.
  • Klabu ya Arsenal ina matumaini ya kumbakiza mshambuliaji wao Pierre-Emerick Aubameyang, 30, ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga na miamba ya Catalunya Fc Barcelona na Real Madrid, ngao kubwa ni uhusiano wa Baba yake na Arsenal.
  • Miamba ya Catalunya Fc Barcelona ina siku thelathini kuanzia leo Jumatano mpaka Julai 7 kuthibitisha kama wataweza kama watakuwa tayari kuvunja kibubu na kutoa Euro milioni 110 (£98m) kwa mshambuliaji wa Inter Milan Lautaro Martinez ambazo ziko kwenye kipengele cha mkataba wake.

Roger Federer kuonekana tena uwanjani 2021
Matumizi ya fedha CHADEMA: Wabunge 69 kuhojiwa TAKUKURU