Mshambuliaji wa Manchaster City, mjerumani Leroy Sane, 24, ametengewa jezi nambari 10 katika kikosi cha Bayern Munich kwa ajili ya msimu ujao. (Mirror).

Chelsea wanapambana kumuuza Victor Moses wakati Inter Milan wakikataa kulipa kitita cha pauni 10.75 milioni, kwa ajili ya winga huyo wa Nigeria , 29.(Sun).

Wakala wa Jorginho, 28, amesisitiza kuwa kiungo wa Italia ana furaha katika kikosi cha Chelsea na kuwa Juventus haijaonesha nia ya kumchukua mchezaji huyo. (Metro).

Mlinda mlango wa Trabzonspors, na anayelengwa na Leicester City mturuki Ugurcan Cakir, 24 ametengewa kiasi cha Euro 20 milioni na klabu ya Sevilla. (Leicestershire live).

Liverpool wako tayari kuwauza wachezaji watatu msimu huu ili kuweza kugharamia uhamisho wa pauni 52 milioni kwa ajili ya mshambuliaji wa miaka 24 wa RB Leipzig, mjerumani Timo Werner. (Athletic).

Manchester United wangependa kumshikilia mshambuliaji, 30, Odion Ighalo,kwa mkopo kutoka Shanghai Shenhua, lakini wamerudi nyuma kuhusu mustakabali wa mchezaji huyo raia wa Nigeria baada ya Marcus Rashford afya yake kuimarika. (Sky Sports).

Arsenal wanafikiria kubadilishana wachezaji na Atletico Madrid kwa mshambuliaji wa kifaransa Alexandre Lacazette ,28 kwenda Hispania, na Thomas Lemar, 24 kwenda Uingereza. (AS-in Spanish).

Neymar  28, hataondoka Paris St-Germain kujiunga tena na Barcelona msimu huu kwa sababu ya athari za virusi vya corona kwa uchumi wa klabu za mpira, ameeleza wakala wa Mbrazili huyo. (Star).

Mizunguko ya awali ya Kombe la Carabao iko kwenye tishio ikiwa msimu ujao haitaanza kabla ya mwanzoni mwa mwezi Septemba. (Telegraph).

Masumbwi kurejea Julai
Video: Polisi -"Hatujifichi na tochi kukomoa madereva"