Uongozi wa timu ya Ferrari inayoshiriki michuano ya mbio za magari, umetangaza taarifa za msiba uliomifika, mkurugenzi wao mtendaji James Allison ambaye amempoteza mkewe.

Kiongozi huyo ambaye ni baba wa watoto watatu, alifunga ndoa na mkewe Rebecca miaka mitatua iliyopita na kabla ya kutangazwa kuwa mkurugenzi mtendaji wa timu, alikua mkurugenzi wa ufundi wa timu ya Ferrari kuanzia mwezi July mwaka 2013.

Timu ya Ferrari, imetangaza kuwa katika hali ya majonzi kufuatia msiba uliomfika bosi wao huyo, mwemnye umri wa miaka 47 ambaye sasa hatokuwepo katika michuano ya Bahrain GP, kutokana na kipindi hiki ambacho atahitaji kupumzika.

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa timu hiyo imesomeka kwamba: “Mwenzetu James Allison, atakuwa katika mapumziko kutokana na msiba wa kumpoteza mke wake kipenzi Rebecca. Sisi kama timu ya Ferrari tunaungana kwa pamoja na mwenzetu katika kipindi hiki kigumu.”

Ozil: Wenger Ni Sababu Kubwa Kwangu Kujiunga Na Arsenal
Luis Suarez Amaliza Kifungo Cha FIFA