Kaimu Mkurugenzi Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Mhandisi Kapulya Musomba amekanusha taarifa zinazoenezwa na kampuni ya Dangote kwamba TPDC imeshindwa kukiuzia gesi asilia kwa bei rahisi kiwanda hicho cha Saruji na hivyo kusababisha kusimamisha uzalishaji wa kiwanda hicho.

Mhandisi Musomba ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akiongea na waandishi wa habari na kutolea ufafanuzi juu ya suala hilo.

“TPDC imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuhakikisha kwamba kampuni ya Dangote inapata nishati hiyo muhimu kwa ajili ya kuzalisha saruji ikiwemo kufanyika kwa vikao mbalimbali pamoja na makubaliano yaliyofanyika kwa Dangote kuridhia nia yao ya kutumia gesi asilia ili kuzalisha umeme kwa ajili ya kiwanda hicho,”Alisema Mhandisi Musomba.

Aidha amesema TPDC inafuata kanuni na utaratibu wa kupanga bei ya gesi asilia ambapo hupanga bei ya gesi asilia ambapo hupanga kulingana na aina ya wateja waliopo katika makundi mbalimbali ingawa bei elekezi ambayo inapendekezwa na TPDC lazima iridhiwe na ipitishwe na EWURA ndipo ianze kutumika.

Hata hivyo amesema kuwa TPDC inawajali wawekezaji wake akiwemo Dangote ili wawekeze katika kukuza uchumi wa nchi.

Breaking News: Lady Jay Dee ayamaliza na Ruge, aruhusu Clouds kupiga nyimbo zake
Waziri Mkuu aongoza viongozi na wananchi kuaga mwili wa mzee Pinda