Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kuhusu kuwepo kwa nafasi wazi ya Ubunge katika Jimbo la Singida Kaskazini kufuatia, Lazaro Samwel Nyalandu kujivua Uanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na hivyo kupoteza sifa ya kuwa Mbunge.
Aidha, kwa mujibu kifungu cha 113(1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume imepokea Hati ya Mahakama Kuu ya Tanzania ikithibitisha uamuzi wa Mahakama hiyo juu ya kutengua matokeo ya Uchaguzi wa Mbunge wa Jimbo la Longido ambalo, Onesmo Ole Nangole alikuwa ni Mbunge.
Wakati huo huo Waziri wa Tamisemi kwa kutumia mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, ameitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata tano zilizopo katika Halmashauri mbalimbali.
Hata hivyo, kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi itatoa ratiba ya Uchaguzi Mdogo wa kujaza nafasi wazi za Majimbo na Kata hizo hapo baadae.
Majimbo na Kata zilizo wazi ni kama ifuatavyo
-
Boti yazama ziwa Victoria ikiwa na watu 17
-
Majaliwa ampa neno Dkt. Kigwangalla
-
Jamii yatahadharishwa kuhusu mvua kubwa
Jedwali Na. 1: Majimbo yaliyowazi
NA. | MKOA | HALMASHAURI | JIMBO |
1. | Singida | Halmashauri ya Wilaya ya Singida | Singida Kaskazini |
2. | Arusha | Halmashauri ya Wilaya ya Longido | Longido |
Jedwali Na. 2: Kata zilizowazi
NA. | MKOA | NA. | HALMASHAURI | NA. | KATA | ||||||
1. | Kagera | 1. | Halmashauri ya Wilaya ya Ngara. | 1 | Keza | ||||||
2. | Arusha | 2 | Halmashauri ya Jiji la Arusha | 2 | Kimandolu | ||||||
3. | Pwani | 3. | Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. | 3 | Kurui | ||||||
4. | Tabora | 4. | Halmashauri ya Wilaya ya Tabora | ||||||||
5 | Kwaguni
|