Klabu ya Tusker FC ya Kenya imejiondoa kwenye Michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame la CECAFA) inayotarajiwa kuanza Agosti 1-14 jijini Dar es Salaam.

Mabadiliko hayo yamelazimisha Kamati ya mashindano ya CECAFA kubadilisha makundi ambayo sasa yatakuwa mawili na timu nne katika kila moja.

Express FC ya Uganda sasa itafungua mashindano kwa mchezo wao wa kwanza wa Saa saba mchana dhidi ya Atlabara FC ya Sudan Kusini mnamo Agosti Mosi, siku hiyo hiyo Young Africans SC itakutana na timu waalikwa, Nyasa Big Bullets FC kutoka Malawi saa 10 jioni; Mechi zote hizo za Kundi A kupigwa dimba la Mkapa.

Yusuf Mosi, Mkurugenzi wa Mashindano wa CECAFA amesema mechi hizo zitachezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa na Azam Complex Chamazi.

Timu mbili bora kutoka kila kundi moja kwa moja zitafuzu kwenye nusu fainali.

KCCA FC ya Uganda ndio mabingwa watetezi wa taji waliloshinda mnamo 2019 huko Kigali, Rwanda kwa kuifunga Azam FC.

KUNDI A: Young Africans (Tanzania), Nyasa Big Bullets (Malawi), Express FC (Uganda), Atlabara FC (Sudan Kusini).

KUNDI B: KCCA FC (Uganda), Azam FC (Tanzania), Le Messager Ngozi (Burundi), KMKM FC (Zanzibar).

Mo Dewji: Usajili Simba ni siri
Mo aweka mzigo, kujenga uwanja