Kupitia mashindano ya ubora wa asali zinazozalishwa barani Afrika, asali kutoka Mkoa wa Tabora ilishika nafasi ya pili (2) kwa ubora.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa Bungeni jijini Dodoma.
Amesema, kutokana na juhudi hizo, asali ya Tanzania imeendelea kuuzwa katika masoko ya nchi za Umoja wa Ulaya, Uarabuni na kwenye masoko mapya ya Poland na China.
Katika hatua nyingine, Waziri Mchengerwa amesema kwa sasa idadi ya Simba nchini imefikia zaidi ya 14,912, na kuifanya Tanzania kuongoza duniani kwa kuwa na Simba wengi kuliko Taifa lolote.