Siku chache baada ya Uganda kuweka wazi kuwa itashirikiana na Tanzania kujenga Bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini humo kuelekea Tanga na sio Kenya, nchi hiyo imetangaza ‘neema’ nyingine ya biashara ya nishati hiyo kati yake na Tanzania.

Akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni, Waziri wa Nishati Waziri wa Maendeleo ya Nishati na Madini wa Uganda, Irene Muloni amesema kuwa nchi yake ina mpango wa kujenga bomba jingine jipya la gesi kupitia njia hiyo, ili kufanya biashara zaidi na Tanzania kupitia njia hiyohiyo.

“Upo uwezekano mkubwa wa kujenga bomba hilo lakini utekelezaji wake utaanza baada ya mradi huu wa bomba la mafuta wa sasa kukamilika, hivyo bado tupo kwenye majadiliano juu ya mpango mpya” Waziri huyo wa Uganda anakaririwa.

Waziri huyo ameongozana na ujumbe wa wataalam wa gesi na mafuta kutoka nchini kwake na wamekutana na Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo kujadili namna ya kutekeleza mpango huo wa ujenzi wa bomba hilo.

Mhongo alieleza kuwa Uganda na Tanzania zimekubaliana kuchangia ujenzi wa mtambo wa kuchakata mafuta ghafi katika mpango huo na kwamba nchi nyingine za Afrika Mashariki zimeridhia kununua mafuta kutoka kwenye mradi huo ili kukuza biashara katika ukanda huo.

 

 

Makonda asema hataki kuwaona wasanii nyumbani kwake, ni baada ya kumpotezea
Serikali Yaahidi kutembea juu ya hoja za Zitto