Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, Jeremy Hunt ameahidi kuendelea kuishinikiza China kuhusu kuacha kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji jijini Hong Kong huku mzozo wa Kidplomasia ukiongezeka.

Hunt amesema kuwa kutakuwa na athari kubwa iwapo China itakiuka makubaliano yalioafikiwa kuhusu haki jijni Hong Kong wakati Uingereza ilipoikabidhi uthibiti.

Akizungumza na BBC radio , Hunt amekataa kutaja hatua maalum zitakazochukuliwa, lakini akasema kuwa hatua hizo zinapaswa kuachwa wazi na kwamba kile alichotaka kufanya ni kuweka ujumbe wazi kuwa hilo sio jambo ambalo litapuuzwa na kuendelea mbele lakini litakuwa suala muhimu sana kwa Uingereza.

Aidha, baada ya onyo la kwanza la Hunt siku ya jumanne la kuchukuwa hatua dhidi ya China , wizara ya mambo ya nje ya China imejibu kwa kumtuhumu Hunt kwa kujiingiza katika nadharia za kikoloni.

Balozi wa China nchini Uingereza, Liu Xiaoming jana alizungumza na waandishi habari na kuitaka Uingereza kukoma kuingilia masuala ya ndani ya Hong Kong, pia ameonya kuwa hatua hiyo inatishia kuendelea kuharibu uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Vyombo vya habari hasa vya serikali ya China vinailaumu Uingereza, Mareknai na nchi nyingine za Magharibi kwa kuwapa kiburi na nguvu waandamanaji.

Mamia ya waandamanaji walilivamia bunge la Hong Kong siku ya Jumatatu baada ya kuidhinisha siku ya kurejeshwa kwa uongozi wa China mwaka 1997 chini ya muundo wa serikali moja na mifumo miwili inayojumuisha uhuru ambao haupatikani China ikiwa ni pamoja na uhuru wa kufanya maandamano.

 

 

Makonda aikaba koo ofisi, 'Nazitaka hizo fedha'
Ashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumlawiti mama yake mzazi