Wananchi wameishauri Serikali kutofumbia macho vitendo viovu na badala yake iweke mkazo mkazo wa kisheria kwa kuwawajibisha wahusika, ambao wamekuwa wakiongezeka kila kukicha huku wengi wao wakitumia kivuli cha utandawazi na ugumu wa maisha kama kigezo.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya Wananchi waliohojiwa na Dar24 Media kwa nyakati tofauti, akiwemo Steven Bukumbi ambaye amesema endapo wasimamiaji wa maadili watatekeleza wajibu wao, ni wazi kuwa Taifa litarejea katika asili yake na kuendelea kuheshimika ulimwenguni.

Steven Mkwawa, Mmoja wa Wananchi waliohojiwa na Dar24 Media.

Amesema, “hali si shwari nchini wizi, ubakaji, ushoga na mengineyo yamekuwa ni mambo ya kawaida lakini cha ajabu Polisi wapo, vyombo vya sheria vipo, Viongozi wa dini wapo, wazazi na walezi wapo na sote eti kwa pamoja tunashangaa.”

Kwa upande wake Maria Nkugwe amesema, kitendo cha baadhi ya watendaji Serikali kutowajibika kunafanya uwepo wa ongezeko la waharibifu wa maadili na kuziomba mamlaka husika kuwa makini kwani madhara yake ni makubwa kwa nyakati zijazo.

“Mambo yakipuuzi yanapewa sana kipaumbele, waweza kuta siku hizi vijana wetu wanafanya mambo ya ajabu lakini watu wanachukulia kawaida, zamani ilichukulika kama mwana wa mwenzio ni wako lakini siku hizi hiyo dhana haipo kwakuwa watenda maovu wana watoto sasa tuchukue hatua mapema sheria zipo zitumike,” amesisitiza Maria.

Mapema hivi karibuni, Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar bin Zubeir bin Ally aliwataka Masheikh na viongozi wa dini kukemea vitendo viovu vinavyomchukiza Mwenyezi MUNGU huku akikemea baadhi ya watu na mataifa yanayohamasisha mapenzi ya jinsia moja.

Ajali: Basi lauwa tisa Katavi, majeruhi wasimulia tukio
Uhalifu mtandaoni: Polisi yajipanga kisayansi