Takwimu za Program ya Ukimwi ya Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa maelfu ya watoto wanakufa kutokana HIV na Ukimwi kinyume na watu wazima, kutokana na kutopatiwa tiba ya ugonjwa huo unaosababisha kifo.
Msemaji wa UNAIDS, Charlotte Spector amesema asilimia 76 ya watu wazima wana fursa ya matibabu lakini kwawatoto ni nusu pekee ambao wanaoishi na HIV ambao wanapatiwa matibabu ili kuokoa maisha na kwamba asilimia 15 ya vifo vyao vyote vinatokanavyo na Ukimwi.
Amesema, “Mwaka jana pekee watoto 160,000 waliambukizwa HIV. Kwa hiyo, kinachotokea ni kwamba nchi 12 zilikuja pamoja barani AFrika kwasababu nchi sita kusini mwa jangwa la Sahara barani humo zinawakilisha asilimia 50 ya wale wenye maambukizi mapya.”
Aidha, nchi 12 za kiafrika zimeungana katika ushirika wa ulimwengu ulioongozwa na UNAIDS, Shirika la Afya Duniani na UNICEF ili kuziba mianya ya tatizo hilo huku Spector akisema Mawaziri wa afya kutoka nchi nane watazindua juhudi hizo wiki ijayo, hapa nchini Tanzania.