Jana, mitandao ya kijamii duniani ilibeba habari nyingine kubwa ya kushtua kuwa bilionea wa madawa ya kulevya, Joaquín Guzmán maarufu kama El Chapo ametoroka tena kwa mara ya tatu kutoka katika jela ya yenye ulinzi mkali.

Habari hizo zilizozua mjadala mkubwa kwenye mitandao hiyo zilianzia kwenye mtandao mkubwa wa Marekani wa hoax ABC News ambao umedaia kupika uzushi unaokaribiana na ukweli na kuusambaza.

Hata hivyo, uongozi wa gereza linalomshikilia umekanusha taarifa hizo ingawa imeeleza kuwa kulikuwa na dalili za mpango mwingine wa kumtorosha bilionea huyo nguli wa biashara haramu ya dawa za kulevya.

Taarifa zilizoripotiwa na USA Today zimeeleza kuwa kumekuwa na juhudi za kila mara kuhakikisha tajiri huyo hatoroki tena ambapo wakuu wa gereza hilo wamekuwa wakimhamisha mara kwa mara kwenye selo anazokaa huku kila njia ya gereza hilo ikiwa na ulinzi mkali.

El Chapo alitoroka kwa mara ya pili kutoka kwenye gereza lenye ulinzi mkali kupitia kwenye bomba la maji machafu lililotokea kwenye bahari.  Hata hivyo, Makomando wa Mexico walifanikiwa kuyafikia maficho yake na kupambana na walinzi wake kabla hawajamkamata tena. Katika zoezi hilo, walinzi wake watano waliuawa na makomando hao.

Wachambuzi wengi wamekuwa wakieleza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa timu ya El Chapo kuratibu jaribio lingine la kumtorosha Boss wao.

Hata hivyo, Reuters na Guardian wameripoti kuwa jana baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa wafanyakazi wa muuza unga huyo walikamatwa katika maeneo mbalimbali nchini Mexico hususan karibu na mpaka wa Arizona.

 

 

 

Serikali yapiga 'stop' shule binafsi kupandisha Ada
Ruby amlilia Ali Kiba, adai amemfananisha na Mbwa