Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ummy Mwalimu amewaagiza wakuu wa Mikoa na wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanafunzi wote wanapumzika wakati wa Likizo.
Waziri Ummy amesema ni vizuri wanafunzi kupata muda wa kujifunza maswala ya kijamii na kitamaduni ikiwa ni pamoja na kazi za nyumbani na kupumzisha akili kabla ya kuanza kwa masomo baada ya likizo.
Waziri Ummy ameongeza pia ni Muhimu wanafunzi wawapo nyumbani kufundishwa maswala ya ujasiriamali kama biashara ili kujua mapema namna ya kutafuta kipato kwa kujitegemea.
Ameyasema hayo katika mahafali ya 29 ya wakala wa maendeleo ya uongozi wa Elimu Bagamoyo ADEM alipokua Mgeni Rasmi.
Hata hivyo waziri Ummy amekemea baadhi ya tabia za uongozi wa shule kadhaa kufanyabelimu kama biashara na kuwatoza wazazi pesa wakati wa likizo kwa kisingizio cha masomo ya ziada.